WASTAAFU 10,000 WA PSSSF WALIOKUWA WANADAI MALIMBIKIZO YA PENSHENI YA MKUPUO NA ILE YA KILA MWEZI WALIPWA BILIONI 880

Friday, June 14, 2019

 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) umefanya malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 880 kwa wastaafu elfu 10,000 ambao walikuwa wanadai malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ya kila mwezi, Meneja Kiongozi wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema.

Amesema malipo hayo yamefanyika katika kipindi cha mpito kilichotolewa na serikali kuanzia Agosti 2018 hadi Februari 2019 hii ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu Mfuko huo uanze kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

“Ili kuhakikisha PSSSF inatoa huduma bora na za haraka, imefungua ofisi mikoa yote Tanzania bara na Visiwani na tunatoa wito sasa, kwa wale wastaafu takriban elfu 10,500 ambao bado taarifa zao hazijahakikiwa wafike kwenye ofisi zilizo karibu nao ili kukamilisha zoezi hilo muhimu linalofanyika kila mwaka.” Alisema Meneja huyo kiongozi wakati akizungumza na waendesha bloggers na waendesha mitandao ya kijamii kwenye ofisi za PSSSF, barabara ya Ohio jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.

Alisema uhakiki wa wastaafu sio kitu kipya ingawa mwaka huu zoezi hilo lilionekana kama ni geni.

“Lengo la uhakiki ni kuupa Mfuko fursa ya kufanya malipo kwa wakati, usahihi na kwa mtu anayepaswa kulipwa kwani taarifa zinaweza kubadilika ikiwa ni pamoja na zile za kibenki huenda muhusika akahama kutoka benki moja kwenda nyingine, mabadiliko ya wategemezi lakini haka kifo pia.” Alifafanua Bi. Chiume.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (katikati), akisikilzia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa bloggers katika kikao baina ya meneja huyo na wamiliki na waendeshaji wa blogu hapa nchini. Kikao hicho kilicholenga kujenga mahusiano na kuutambulisha Mfuko huo Mpya kwa wamiliki hao wa mitandao ya kijamii kilifanyika ofisi za PSSSF jengo la Jubilee Tower jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akizungumza.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akizungumza.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi(kulia), akitoa maoni yake wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi. 
Bi. Eunice Chiume (kushoto), akimsikilzia Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi (watatu kushoto), wakati wa kikao hicho.
Bi. Eunice Chiume, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network, (TBN) Bw. Joachim Mushi, wakati wa kikao hicho.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (watatu kushoto) na Afisa Uhusiano Mewandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wakwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Bloggers mara baada ya kikao hicho.

RC MAKONDA AONGEA NA BLOGGERS KWA SIMU

Wednesday, December 07, 2016

 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam aongea kwa njia ya simu katika Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es salaam Desemba 6, 2016


Waziri Nape Afunga Mkutano Mkuu Wa Waandishi Wa Habari Za Mitandao (TBN), Aahidi Kuanzisha Tuzo.

Wednesday, December 07, 2016

  Na Beatrice Lyimo, Maelezo

Serikali inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar  es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Aidha, Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na   makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.
Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
“Tutumie fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tiunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa Ufafanuzi wakati alipokuwa akieleza namna ya kuitambua mitandao ya Kijamii pamoja na uanzishaji wa Tuzo kwa Waendeshaji mitandao hiyo.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza mapema leo jijini Dar wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) iliokwenda sambamba na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.Picha na Michuzi Jr.
Mwenyekiti wa Muda wa chama cha Waendesha mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network-TBN,Joachim Mushi akimkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kufunga mkutano huo na pia kuyotolea ufafanuzi baadhi ya mambo
.


Mmoja wa Wajumbe wa mkutano huo na blogger na mwanamuziki mkongwe  John Kitime ambaye amebobea katika mambo ya Hakimiliki, akitoa elimu ya mambo ya Hakimiliki kwa washiriki wa mkutano huo.

Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea.

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TBN WAFUNGULIWA DAR, SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII

Tuesday, December 06, 2016

 Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar


SERIKALI imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Blogs) kuwa chombo rasmi cha habari nchini. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas,  wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka na Mafunzo ya Tanzania Bloggers Network (TBN), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana Jumatatu.

"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema  Dkt. Abbas.

Dkt. Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.
Katika hatua nyingine Dkt. Abbas alisema Blogs hazina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weledi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine.
Dkt. Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana  asubuhi. 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.

 Mkurugenzi Mkuu wa mtandao wa Jamii Forums Bw. Maxence Melo akitoa moja ya somo katika mafunzo hayo.


 Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano,mafunzo hayo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

BLOGGERS TANZANIA WAPEWA MAFUNZO YA NAMNA BORA YA UENDESHAJI WA MITANDAO YA KIJAMII

Monday, December 05, 2016

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Dk. Hassan Abbas (wa pili kulia) akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu wa siku mbili wa Tanzania Bloggers Network (TBN) uliofanyika katika ukumbi wa PSPF jijini Dar,pichani kulia ni Kaimu Meneja Mwandamizi kutoka benki ya NMB,Stephen Adili.
Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi(aliyesimama)  akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari  MAELEZO, Dkt.Hassan Abbas  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tanzania Bloggers Network(TBN) uliofanyika katika ukumbi wa PSPF jijini Dar leo.

Baadhi ya Bloggers wakiwa kwenye mkutano wao unaoendelea hivi sasa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NMB WADHAMINI MKUTANO WA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN)

Friday, December 02, 2016

 Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu wa TBN,Khadija Khalili na Mwisho kushoto ni Meneja wa Mitandao wa NMB,Joyce Nsekela.


Akizungumza  mbele ya Wanahabari  mapema leo (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN),Joachim Mushi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 na 6 ,2016 hapa hapa jijini Dar,ambao utawashirikisha wanachama wapatao 150 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Mushi alisema kuwa katika mkutano huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh Nape Mosses Nnauye,

"Mgeni rasmi anaetarajiwa kufungua mkutano huo ni  Waziri Nape Nnauye,lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kupeana elimu na kubadilishana mawazo  juu ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili  na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji",alisema Mushi.

Alisema kuwa uendeshaji wa Mitandao baadhi yao wanaifanya ni kama ajira nyingine,hivyo kimsingi lazima wakubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani,hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya  ya mitandao hii,

 Mkutano huo utakaokuwa wa aina yake na kuiandika historia tangu kuanza kwa mitandano ya Kijamii hapa nchini,umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola
Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale akizungumzia udhamini wa benki ya NMB katika mkutano mkuu wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili na kuwakutanisha bloggers kutoka Tanzania Bara na Visiwani.   
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi(wa pili kutoka kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale kwa ajili ya kudhamini mkutano huo.

BLOGGERS WATINGA BUNGENI KWA MWALIKO WA WAZIRI NAPE

Saturday, May 14, 2016

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Blogs (Bloggers) aliowaalika wakati wa kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Annastazia Wambura. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Baadhi ya Bloggers wakiwa bungeni wakati wa Bajeti ya wizara hiyo
Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ akisoma taarifa ya maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo.
Baadhi ya Bloggers wakisikiliza mwenendo wa bunge. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Wamiliki wa Blogs Tanzania a.k.a Tanzania Bloggers Network (TBN), Bw. Joachim Mushi.
Nape akiwa na Bloggers pamoja na wasanii bungeni Dodoma

VIONGOZI WAANDAMIZI WA TBN Wakutana Na Maafisa Wa Ubalozi Wa Marekani

Friday, August 14, 2015

 

Viongozi waandamizi wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakigonganisha glasi na Afisa Mahusiano ya Umma wa Ubalozi wa Marekani Bi. Marissa Maurer (wa tatu kushoto) na Afisa wa Siasa na Uchumi wa ubalozi huo Bw. Vincent Spera (wa pili kushoto) walipokutana jijini Dar es salaam kwa mazungumzo yasiyo rasmi ili kubadilishana mawazo ya njia bora ya kuendeleza tasnia hiyo ya habari za mtandao inayokuja juu kwa kasi nchini. 
TBN ni umoja wa bloggers wapatao 100 waliouunda ili kujiendeleza na kusimamia maslahi yao huku wakisaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa nay a tasnia ya habari kwa jumla. Wengine toka kulia ni wajumbe wa TBN Max Mello, Joachim Mushi (Mwenyekiti), Monica Mara (Afisa Mipango), Hadija Kalili  (Katibu), Shamim Mwasha (mtunza hazina) na Afisa habari wa ubalozi huo Japhet Sanga. Picha kwa hisani ya TBN

MNUSO WA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) MEET AND GREET PARTY WAFANA SANA DAR ES SALAAM SERENA HOTEL JIJINI DAR

Sunday, March 01, 2015

 

Sehemu ya Wamiliki wa Blogs mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers Network,ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg. Kajubi Mukajanga pamoja na baadhi ya wadhamini waliofanikisha hafla hiyo,iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers Network,Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg. Kajubi Mukajanga (wa pili kulia) akizungumza jambo na baadhi ya Wamiliki wa Blogs Tanzania,waliokutana pamoja leo kwa lengo la kufahamina na kuunganisha vyema umoja wao.

Mkurugenzi wa Masoko kwa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu,Kelvin Twissa akizungumza machache katika hafla hiyo. 

AU 
 
Designed By TBN | Developed By Gadiola Emanuel