Serikali inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Aidha, Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.
Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
“Tutumie fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tiunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa Ufafanuzi wakati alipokuwa akieleza namna ya kuitambua mitandao ya Kijamii pamoja na uanzishaji wa Tuzo kwa Waendeshaji mitandao hiyo.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza mapema leo jijini Dar wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) iliokwenda sambamba na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.Picha na Michuzi Jr.
Mwenyekiti wa Muda wa chama cha Waendesha mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network-TBN,Joachim Mushi akimkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kufunga mkutano huo na pia kuyotolea ufafanuzi baadhi ya mambo .
Mmoja wa Wajumbe wa mkutano huo na blogger na mwanamuziki mkongwe John Kitime ambaye amebobea katika mambo ya Hakimiliki, akitoa elimu ya mambo ya Hakimiliki kwa washiriki wa mkutano huo. Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Mtandao wa Wana Blogu wa Tanzania (TBN) ni jamii yenye nguvu ya waendesha blogu wa Kitanzania walio ndani ya nchi pamoja na walio katika Diaspora. TBN iliundwa rasmi Aprili 2, 2015, chini ya Sheria ya Tanzania ya Mashirika (CAP. 337 R.E. 2002) na kupata Cheti cha Usajili namba S.A. 20008 cha Tarehe 02 Aprili, 2015 kutoka kwa Msajili wa Taasisi zisizo za Kiserikali katika Wizara ya Mambo ya Ndani.
DHAMIRA
Dhamira ya TBN ni kuhakikisha kuwa wanachama wake wanafanya kazi kwa maono
yanayolingana na malengo makuu ya mtandao huu. Lengo letu ni kukuza weledi na
athari ya tasnia ya blogu ndani ya jamii yetu.
MALENGO
Lengo letu ni kuweka nyenzo muhimu
ya kutumikia Tanzania na watu wake kwa weledi.
VIONGOZI WA TBN
Lengo letu ni kuweka nyenzo muhimu
ya kutumikia Tanzania na watu wake kwa weledi.
DKT. MWIGULU AWAONYA WAVUNJIFU WA SHERIA
-
*WAZIRI MKUU *Dkt. Mwigulu Nchemba amevitaka vyombo vinavyosimamia usalama
barabarani vitekeleze sheria hizo bila upendeleo kwani tabia ya kuogopana
na ...
Post a Comment