HABARI MPYA

Mwanachama wa TBN Veronica Mrema atajwa tuzo ya ISU Elihle 2026 - Afrika

Saturday, August 08, 2026


Veronica%20Mrema


Na Mwandishi Wetu


Mtanzania Veronica Mrema , mwanachama wa Mtandao wa Mabloga Tanzania , TBN, anayeendesha jukwaa la kidijiti la  M24 TANZANIA MEDIA ni miongoni mwa waandishi wa  habari sita  waliochaguliwa kuendelea na mchakato wa tuzo za ISU Elihle kwa mwaka 2026 Barani Afrika.

Veronica ametajwa katika orodha hiyo baada ya wazo lake la habari kuhusu watoto wanaoishi na ugonjwa wa Siko Seli kupitiwa, na kuonekana ni bora.

Jopo la majaji wa tuzo hizo limesema kulikuwa na mawazo 155 ambayo walipokea kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Hatua ya Veronica kutajwa kwenye tuzo hiyo inaongeza rekodi nzuri katika uandishi wa habari za afya na maendeleo na kuiweka Tanzania katika nafasi ya kuendelea kutoa waandishi wa habari wanaotumia kalamu zao kuibua changamoto za watoto na kuchochea mabadiliko yenye manufaa kwa jamii.

Kupitia wazo lake lililochaguliwa Veronica atafanya uchunguzi na kuibua simulizi kuhusu mzigo unaoongezeka wa ugonjwa wa Siko Seli miongoni mwa watoto nchini Tanzania, akiangazia kwa kina namna ugonjwa huo unavyoathiri maisha ya watoto, kuanzia afya zao, lishe, elimu, ukuaji wa kimwili, pamoja na ustawi wao wa kihisia na kisaikolojia. 

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, idadi ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa Siko Seli nchini imeongezeka kutoka takribani watoto 8,000 hadi 14,000 kila mwaka, hali inayoifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye mzigo mkubwa wa ugonjwa huo Afrika na duniani. 

Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi tatu zenye idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo Barani Afrika kila mwaka huku ikishika nafasi ya nne duniani.

Pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna watoto bado hukumbana na changamoto za kuchelewa kugundulika, ukosefu wa huduma maalum za matibabu na uelewa mdogo wa jamii kuhusu ugonjwa huo.

Veronica atakusanya simulizi za watoto wanaoishi na Siko Seli, wazazi na walezi wao, wataalamu wa afya, wataalamu wa lishe pamoja na watunga sera, kwa lengo la kuonesha hali halisi ya maisha yao na kuibua suluhisho zinazoweza kuboresha afya na ustawi wa watoto hao.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa washindi, Veronica amesema amepokea kwa heshima kubwa kutajwa katika orodha hiyo ya ISU Elihle.

"Ni fursa ya kuendelea kutumia uandishi wa habari kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

"Kuchaguliwa miongoni mwa waandishi sita kutoka kazi 155 zilizowasilishwa ni heshima kubwa kwangu na kwa Tanzania. Lakini zaidi ya yote, ni nafasi ya kuhakikisha sauti za watoto wanaoishi na Siko Seli zinasikika.

"Ninaamini simulizi hizi zitasaidia kuongeza uelewa wa jamii na kuhimiza uwekezaji zaidi katika uchunguzi wa mapema, huduma za afya na lishe kwa watoto hawa," amesema.

Ameongeza atatumia uandishi wa habari unaozingatia ushahidi, takwimu na simulizi za wahusika ili kuonesha changamoto halisi zinazowakabili watoto wenye Siko Seli na kuibua mijadala itakayochochea maboresho ya sera na huduma za afya.

ISU Elihle Award inalenga kuhamasisha uandishi wa habari unaoweka watoto katikati ya simulizi na unaochochea mijadala yenye kuleta mabadiliko ya sera, uwajibikaji na hatua za kuboresha ustawi wa watoto barani Afrika.

Pamoja na Veronica Mrema wa Tanzania, washindi wengine wa ISU Elihle Award 2026 ni David Arome wa The Development Report (Nigeria) na Hind Fawzi wa Medina FM (Morocco), Rakiya Mohamed wa Blueprint (Nigeria), Wezzie Joy Gausi wa Times Group (Malawi) na Kelvin Tambo wa Capital Radio (Malawi).

Kupitia tuzo hiyo, washindi watapata fursa ya kutekeleza miradi yao ya uandishi kwa msaada wa wahariri na wataalamu wa uandishi wa habari, pamoja na ushauri wa kitaalamu (mentorship) ili kuhakikisha simulizi hizo zinafikia viwango vya juu vya ubora na kuleta athari chanya kwa jamii.

Katika hatua hii, pia watapewa kiasi cha R.10,000 ili kwenda kutekeleza miradi ya uandishi wa makala kulingana na mawazo yao ya habari ambayo waliyawasilisha katika mchakato huo wa kwanza.

Baadae kazi zao zitapitia mchakato wa awamu ya pili ambapo zitashindanishwa ili kupata washindi watatu bora, miongoni mwao.

NEEMA YA KIDIJITALI: SERIKALI YASHUSHA ADA KWA WANABLOGU , TCRA YAZINDUA REDIO YA KISASA 'DSB'

Saturday, February 21, 2026

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji  

****

SERIKALI imetangaza neema ya kihistoria kwa wanablogu, vijana wabunifu, na watoa maudhui mtandaoni nchini kwa kupunguza ada za leseni kwa kiwango kikubwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kurasimisha shughuli za wahabarishaji wa mitandao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini.


Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) jijini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema ada ya leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh50,000 tu, huku ada ya maombi ikiwa ni Sh10,000 pekee.

Mageuzi hayo pia yamegusa kundi la wakusanyaji wa maudhui (Online Content Aggregators), ambao ada yao imeshushwa kutoka Sh1,000,000 hadi Sh100,000 pekee. Aidha, kundi la "Amateteur" limeanzishwa kwa ajili ya vijana wanaochipukia ili waweze kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila vikwazo vya kifedha.

Mapinduzi ya Teknolojia ya DSB

Wakati neema hiyo ikitangazwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, ametangaza kuanza kwa teknolojia mpya ya utangazaji wa redio ya kidijitali nchini inayojulikana kama Digital Sound Broadcasting (DSB).

Teknolojia hiyo itaanza kufanya kazi katika mikoa mitano ya majaribio ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, na Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa sauti na huduma za utangazaji nchini.

"Tumekamilisha maandalizi yote ya kiudhibiti na watoa huduma wa miundombinu wameshapatikana. Hii ni hatua kubwa ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani na kuimarisha utangazaji, hususan maeneo ya vijijini," alisema Dkt. Bakari.


Utafiti: Redio Bado ni Kinara

Katika mkutano huo, Injinia Andrew Kisaka wa TCRA amewasilisha matokeo ya utafiti wa hali ya utangazaji kwa mwaka 2025/2026, ukionyesha kuwa redio inaendelea kuwa chanzo kikuu cha habari kwa asilimia 85 ya Watanzania.

 Hata hivyo, utafiti huo umebaini ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti miongoni mwa vijana, ambapo asilimia 45 hupata habari kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kusikiliza redio au kutazama televisheni.

Upande wa televisheni, utafiti unaonyesha asilimia 65 ya watazamaji wanatumia ving'amuzi, huku maudhui ya ndani yakipendwa zaidi kwa asilimia 70. Serikali imewahimiza watoa huduma za kienyeji kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali (OTT) ili kukidhi mahitaji ya soko la sasa.



Ulinzi wa Hakimiliki na Mikopo

Ili kuhakikisha wanahabari wa kidijitali wanufaika na kazi zao, Serikali imezielekeza taasisi za COSOTA na TCRA kuandaa mpango wa kulinda hakimiliki na kudhibiti uharamia mtandaoni. Aidha, Serikali imeanza kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa watengeneza maudhui kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi.

Hadi kufikia Desemba 2025, TCRA imetoa jumla ya leseni 707 za utangazaji, zikiwemo 318 za maudhui mtandaoni, jambo linaloashiria kukua kwa uhuru wa habari na demokrasia nchini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.





<<<<<<<<<<<<<<<<<<<< >>>>>>>>>>>>>>>>

Serikali  imetangaza neema ya kihistoria kwa wanablogu, vijana wabunifu, na watoa maudhui mtandaoni nchini kwa kupunguza ada za leseni kwa kiwango kikubwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kurasimisha shughuli za wahabarishaji wa mitandao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) Jijini Dodoma tarehe 12 Februari  2026 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema Ada ya Leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh.50,000 tu, huku ada ya maombi ikiwa ni Sh.10,000 pekee.

Mageuzi hayo pia yamegusa kundi la wakusanyaji wa maudhui mtandaoni  (Online Content Aggregators), ambao ada yao imeshushwa kutoka Sh1,000,000 hadi Sh100,000 pekee. Aidha, kundi la "Amateteur" limeanzishwa kwa ajili ya vijana wanaochipukia ili waweze kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila vikwazo vya kifedha.

Mapinduzi ya Teknolojia ya DSB

Wakati neema hiyo ikitangazwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, ametangaza kuanza kwa teknolojia mpya ya utangazaji wa Redio ya kidijitali nchini inayojulikana kama Digital Sound Broadcasting (DSB).


Teknolojia hiyo itaanza kufanya kazi katika Mikoa mitano ya majaribio ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, na Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa sauti na huduma za utangazaji nchini.

"Tumekamilisha maandalizi yote ya kiudhibiti na watoa huduma wa miundombinu wameshapatikana. Hii ni hatua kubwa ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani na kuimarisha utangazaji, hususan maeneo ya Vijijini," amesema Dkt. Bakari.


Utafiti: Redio Bado ni Kinara

Katika mkutano huo, Mhandisi Andrew Kisaka wa TCRA amewasilisha matokeo ya utafiti wa hali ya utangazaji kwa mwaka 2025/2026, ukionyesha kuwa redio inaendelea kuwa chanzo kikuu cha habari kwa asilimia 85 ya Watanzania. Hata hivyo, utafiti huo umebaini ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti miongoni mwa vijana, ambapo asilimia 45 hupata habari kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kusikiliza redio au kutazama Televisheni.

Upande wa Televisheni, utafiti unaonyesha asilimia 65 ya watazamaji wanatumia ving'amuzi, huku maudhui ya ndani yakipendwa zaidi kwa asilimia 70. 

Serikali imewahimiza watoa huduma za kienyeji kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya Kidijitali (OTT) ili kukidhi mahitaji ya soko la sasa.

Ulinzi wa Hakimiliki na Mikopo

Ili kuhakikisha wanahabari wa kidijitali wanufaika na kazi zao, Serikali imezielekeza taasisi za COSOTA na TCRA kuandaa mpango wa kulinda hakimiliki na kudhibiti uharamia mtandaoni. Aidha, Serikali imeanza kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa watengeneza maudhui kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi.

Hadi kufikia Desemba 2025, TCRA imetoa jumla ya Leseni 707 za utangazaji, zikiwemo 318 za maudhui mtandaoni, jambo linaloashiria kukua kwa uhuru wa habari na demokrasia nchini chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<PICHA ZA MATUKIO>>>>>>>>>>>

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI 2026 UKIENDELEA DODOMA

Matukio mbalimbali yakiendelea wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), unaofanyika katika Ukumbi wa New Generation, jijini Dodoma, Februari 12 na 13, 2026, ukiwa na kaulimbiu isemayo ‘Matumizi ya Teknolojia katika Kupanua na Kuboresha Huduma za Utangazaji Vijijini.’ Mkutano huo unalenga kujadili na kutathmini maendeleo ya sekta ya utangazaji nchini, pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha utoaji wa huduma, hususan katika maeneo ya vijijini.

 Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog















































































 
Designed By TBN | Developed By Gadiola Emanuel