Showing posts with label TEKNOLOJIA. Show all posts
Showing posts with label TEKNOLOJIA. Show all posts

PSSSF na Tanzania Bloggers Network (TBN) Kuimarisha Ushirikiano wa Utoaji Elimu ya Hifadhi ya Jamii

Friday, September 11, 2026


Katika hatua inayolenga kupanua wigo wa utoaji wa elimu kwa umma, timu ya maofisa wa juu kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imefanya ziara rasmi katika Makao Makuu ya Muda ya Tanzania Bloggers Network (TBN), yaliyopo Kijitonyama, Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kimkakati na viongozi wa mtandao huo.


Mazungumzo hayo yalilenga kujenga ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili, hususan katika masuala ya habari, uelimishaji wa umma na usambazaji wa taarifa na maarifa sahihi kuhusu mifumo ya hifadhi ya jamii, pensheni pamoja na uwekezaji unaofanywa na PSSSF.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa TBN, Beda Msimbe, alisema mtandao huo uko tayari kutumia majukwaa yake kusimama kidete katika kutoa elimu na kusambaza taarifa sahihi kwa umma, hususan kupitia majukwaa ya kidijitali.

Hata hivyo, alisisitiza umuhimu wa wanachama wa TBN kupata mafunzo ya kina kuhusu shughuli, huduma na uendeshaji wa PSSSF, ili waweze kuwaelimisha wananchi kwa ufanisi na kwa usahihi zaidi.

“Ni muhimu kwanza sisi wanachama wa TBN kupata elimu ya kutosha kuhusu mfuko huu, ili elimu tutakayokwenda kuwapa wananchi iwe sahihi, yenye uelewa mpana na yenye tija,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa msafara wa PSSSF, Abdul Njaidi, alisema ziara hiyo imelenga kujenga uhusiano wa karibu na wadau wa sekta ya habari, pamoja na kuimarisha juhudi za kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii.

Njaidi aliwahakikishia viongozi wa TBN kuwa hoja na mapendekezo yote yaliyowasilishwa katika mkutano huo yatafanyiwa kazi, akisisitiza kuwa ushirikiano huo unalenga kuhakikisha wananchi wanapata uelewa mpana na sahihi kuhusu masuala ya pensheni na uwekezaji unaofanywa na PSSSF.

Naye Mdhamini wa TBN, Issa Michuzi, alisema mtandao huo wenye historia kubwa katika tasnia ya habari za mtandaoni unajivunia weledi na ufanisi katika kutekeleza majukumu yake.

Alisema TBN ipo kwa ajili ya kuhakikisha Tanzania inasomeka vyema katika medani za kidijitali, kwa kutoa taarifa zenye kujenga na kuchochea maendeleo ya taifa.

“Tunataka kuhakikisha Tanzania inasomeka vyema katika medani za kidijitali na kwamba taarifa zinazotolewa zinakuwa na mchango katika kuchochea na kutanua zaidi gurudumu la maendeleo ya taifa,” alisema Michuzi.

Kwa upande wake, Katibu wa TBN, Rahel Pallangyo, alisema mtandao huo uko tayari kutoa waandishi wake mahiri na kutumia majukwaa yake mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, za kuaminika na zenye tija kwa jamii.

Alisema ushirikiano huo utasaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii na kuwawezesha wadau mbalimbali kuelewa kwa kina huduma na fursa zinazotolewa na PSSSF.

Ushirikiano huo unatazamiwa kufungua ukurasa mpya katika matumizi ya vyombo vya habari vya mtandaoni katika kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi wengi zaidi nchini.

Katika mkutano huo, ujumbe wa PSSSF ulioongozwa na Abdul Njaidi ulihusisha pia maofisa Regina Kumba, Grayson Mgunda na Doreen Lyimo.

Kwa upande wa TBN, viongozi walioshiriki mkutano huo ni Mwenyekiti Beda Msimbe, Katibu Rahel Pallangyo, Mtaalamu wa Mawasiliano Cathbert Kajuna na Mdhamini wa TBN, Issa Michuzi.








NEEMA YA KIDIJITALI: SERIKALI YASHUSHA ADA KWA WANABLOGU , TCRA YAZINDUA REDIO YA KISASA 'DSB'

Saturday, February 21, 2026

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji  

****

SERIKALI imetangaza neema ya kihistoria kwa wanablogu, vijana wabunifu, na watoa maudhui mtandaoni nchini kwa kupunguza ada za leseni kwa kiwango kikubwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kurasimisha shughuli za wahabarishaji wa mitandao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini.


Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) jijini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema ada ya leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh50,000 tu, huku ada ya maombi ikiwa ni Sh10,000 pekee.

Mageuzi hayo pia yamegusa kundi la wakusanyaji wa maudhui (Online Content Aggregators), ambao ada yao imeshushwa kutoka Sh1,000,000 hadi Sh100,000 pekee. Aidha, kundi la "Amateteur" limeanzishwa kwa ajili ya vijana wanaochipukia ili waweze kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila vikwazo vya kifedha.

Mapinduzi ya Teknolojia ya DSB

Wakati neema hiyo ikitangazwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, ametangaza kuanza kwa teknolojia mpya ya utangazaji wa redio ya kidijitali nchini inayojulikana kama Digital Sound Broadcasting (DSB).

Teknolojia hiyo itaanza kufanya kazi katika mikoa mitano ya majaribio ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, na Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa sauti na huduma za utangazaji nchini.

"Tumekamilisha maandalizi yote ya kiudhibiti na watoa huduma wa miundombinu wameshapatikana. Hii ni hatua kubwa ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani na kuimarisha utangazaji, hususan maeneo ya vijijini," alisema Dkt. Bakari.


Utafiti: Redio Bado ni Kinara

Katika mkutano huo, Injinia Andrew Kisaka wa TCRA amewasilisha matokeo ya utafiti wa hali ya utangazaji kwa mwaka 2025/2026, ukionyesha kuwa redio inaendelea kuwa chanzo kikuu cha habari kwa asilimia 85 ya Watanzania.

 Hata hivyo, utafiti huo umebaini ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti miongoni mwa vijana, ambapo asilimia 45 hupata habari kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kusikiliza redio au kutazama televisheni.

Upande wa televisheni, utafiti unaonyesha asilimia 65 ya watazamaji wanatumia ving'amuzi, huku maudhui ya ndani yakipendwa zaidi kwa asilimia 70. Serikali imewahimiza watoa huduma za kienyeji kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali (OTT) ili kukidhi mahitaji ya soko la sasa.



Ulinzi wa Hakimiliki na Mikopo

Ili kuhakikisha wanahabari wa kidijitali wanufaika na kazi zao, Serikali imezielekeza taasisi za COSOTA na TCRA kuandaa mpango wa kulinda hakimiliki na kudhibiti uharamia mtandaoni. Aidha, Serikali imeanza kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa watengeneza maudhui kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi.

Hadi kufikia Desemba 2025, TCRA imetoa jumla ya leseni 707 za utangazaji, zikiwemo 318 za maudhui mtandaoni, jambo linaloashiria kukua kwa uhuru wa habari na demokrasia nchini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.





<<<<<<<<<<<<<<<<<<<< >>>>>>>>>>>>>>>>

Serikali  imetangaza neema ya kihistoria kwa wanablogu, vijana wabunifu, na watoa maudhui mtandaoni nchini kwa kupunguza ada za leseni kwa kiwango kikubwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kurasimisha shughuli za wahabarishaji wa mitandao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) Jijini Dodoma tarehe 12 Februari  2026 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema Ada ya Leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh.50,000 tu, huku ada ya maombi ikiwa ni Sh.10,000 pekee.

Mageuzi hayo pia yamegusa kundi la wakusanyaji wa maudhui mtandaoni  (Online Content Aggregators), ambao ada yao imeshushwa kutoka Sh1,000,000 hadi Sh100,000 pekee. Aidha, kundi la "Amateteur" limeanzishwa kwa ajili ya vijana wanaochipukia ili waweze kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila vikwazo vya kifedha.

Mapinduzi ya Teknolojia ya DSB

Wakati neema hiyo ikitangazwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, ametangaza kuanza kwa teknolojia mpya ya utangazaji wa Redio ya kidijitali nchini inayojulikana kama Digital Sound Broadcasting (DSB).


Teknolojia hiyo itaanza kufanya kazi katika Mikoa mitano ya majaribio ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, na Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa sauti na huduma za utangazaji nchini.

"Tumekamilisha maandalizi yote ya kiudhibiti na watoa huduma wa miundombinu wameshapatikana. Hii ni hatua kubwa ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani na kuimarisha utangazaji, hususan maeneo ya Vijijini," amesema Dkt. Bakari.


Utafiti: Redio Bado ni Kinara

Katika mkutano huo, Mhandisi Andrew Kisaka wa TCRA amewasilisha matokeo ya utafiti wa hali ya utangazaji kwa mwaka 2025/2026, ukionyesha kuwa redio inaendelea kuwa chanzo kikuu cha habari kwa asilimia 85 ya Watanzania. Hata hivyo, utafiti huo umebaini ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti miongoni mwa vijana, ambapo asilimia 45 hupata habari kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kusikiliza redio au kutazama Televisheni.

Upande wa Televisheni, utafiti unaonyesha asilimia 65 ya watazamaji wanatumia ving'amuzi, huku maudhui ya ndani yakipendwa zaidi kwa asilimia 70. 

Serikali imewahimiza watoa huduma za kienyeji kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya Kidijitali (OTT) ili kukidhi mahitaji ya soko la sasa.

Ulinzi wa Hakimiliki na Mikopo

Ili kuhakikisha wanahabari wa kidijitali wanufaika na kazi zao, Serikali imezielekeza taasisi za COSOTA na TCRA kuandaa mpango wa kulinda hakimiliki na kudhibiti uharamia mtandaoni. Aidha, Serikali imeanza kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa watengeneza maudhui kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi.

Hadi kufikia Desemba 2025, TCRA imetoa jumla ya Leseni 707 za utangazaji, zikiwemo 318 za maudhui mtandaoni, jambo linaloashiria kukua kwa uhuru wa habari na demokrasia nchini chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<PICHA ZA MATUKIO>>>>>>>>>>>

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI 2026 UKIENDELEA DODOMA

Matukio mbalimbali yakiendelea wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), unaofanyika katika Ukumbi wa New Generation, jijini Dodoma, Februari 12 na 13, 2026, ukiwa na kaulimbiu isemayo ‘Matumizi ya Teknolojia katika Kupanua na Kuboresha Huduma za Utangazaji Vijijini.’ Mkutano huo unalenga kujadili na kutathmini maendeleo ya sekta ya utangazaji nchini, pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha utoaji wa huduma, hususan katika maeneo ya vijijini.

 Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog















































































 
Designed By TBN | Developed By Gadiola Emanuel