HABARI MPYA

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akutana Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam

Thursday, November 27, 2025

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akizungumza na Waandishi wa Habari wa Mtandaoni pamoja na Wanablogu mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kupokea maoni yao, ikiwa ni mfululizo wa mikutano na wadau wa Tasnia ya Habari kwa ajili ya kuboresha masuala mbalimbali ya Mawasiliano baina ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na Vyombo vya Habari, tarehe 27 Novemba, 2025.
Viongozi mbalimbali wakizungumza katika Kikao cha pamoja cha Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, Wanablogu mbalimbali pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Novemba, 2025.

Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali wakizungumza katika Kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Novemba, 2025. 

TBN YAINGIA MCT RASMI: Mwenyekiti Asema Uanachama ni Njia ya Kulinda Weledi na Uhuru

Friday, September 26, 2025

Na Mwandishi wetu

Tanzania Bloggers Network (TBN) imepiga hatua kubwa katika kutambulika rasmi baada ya kukabidhiwa hati za uanachama katika Mkutano Mkuu wa 27 wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), uliofanyika Septemba 25, 2025, jijini Dar es Salaam. TBN ilikuwa miongoni mwa wanachama wapya wanane (8) waliojiunga na Baraza.

Akizungumza baada ya makabidhiano, Mwenyekiti wa TBN, Ndugu Beda Msimbe, alisema kuna manufaa makubwa kwa wanablogu kujiunga na MCT.

"Uanachama huu unatoa uhalali na kutambuliwa rasmi kwa wanablogu mbele ya jamii, Serikali na wadau wengine. Tunajumuishwa katika familia kubwa ya vyombo vya habari vinavyojisimamia, na sasa wanablogu wanatambulika kama chanzo cha habari kinachowajibika," alisema Ndugu Msimbe.

Aliongeza kuwa, TBN sasa inafaidika na mfumo wa ulinzi wa Baraza, hasa katika masuala ya usuluhishi dhidi ya malalamiko. Alisisitiza kuwa mfumo huo utawalinda wanablogu kisheria na kiuchumi dhidi ya vitisho au uwezekano wa kufilisiwa kutokana na faini za kimahakama, kwa kuwa sasa wana kimbilio katika Kamati ya Maadili ya MCT.

Upanuzi huu unakwenda sambamba na wito uliotolewa na uongozi wa MCT unaosisitiza umuhimu wa mshikamano wa wanachama.

Katibu Mtendaji wa MCT, Bw. Ernest Sungura, alikumbusha kwamba kauli mbiu ya mkutano, “Uhai wa Wanachama ni Nguvu na Usalama wa Taaluma ya Habari,” inapaswa kuwa mwongozo.

"Ikumbukwe ni wanachama waliosema siku moja tujisimamie au lah tukubali kufa... Uhai wa wanachama upo katika kushiriki vikao na kulipa ada za uanachama," alisema Bw. Sungura, akionya kuwa enzi za kudhani wafadhili watatoa fedha kwa MCT zimekwisha, na hivyo uhai wa Baraza unategemea wanachama.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Ndugu Yusuf Khamis Yusuf, alisisitiza kuwa katika miaka hii 30 ya MCT tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995, Baraza limejipambanua kama taasisi huru inayolinda weledi na maadili.

Weledi na Uhuru: Njia ya Baraka

Akifungua rasmi Mkutano huo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, Rais Mstaafu wa Nne wa Baraza, alisisitiza kuwa uwepo wa MCT umeokoa vyombo vingi vya habari kutokana na kufilisiwa.

Alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila chombo cha habari, ikiwemo TBN, kuwa kiungo cha ukweli bila kuegemea upande mmoja. Alitahadharisha wanahabari akisema: "Kusimama kwenye haki ni kugumu kuliko kujipendekeza. Kusimama na haki kunahitaji sadaka. Siyo njia nyepesi au rahisi, lakini ni njia ya baraka mno na ni njia inayompendeza Mungu."

Jaji Mihayo pia alizindua rasmi Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT 2025) ambazo zitaendeshwa kwa mfumo wa kidijitali sambamba na tovuti mpya ya MCT, hatua inayodhihirisha dhamira ya Baraza kukuza weledi katika tasnia nzima.

TBN Yajumuika na Viongozi wa Habari Kuelekea Uchaguzi 2025

Sunday, August 24, 2025

 IMG-20250821-WA0058

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Mwaluko Kabudi (wa nne kutoka kushoto waliokaa), akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wadau wa sekta ya habari na utangazaji baada ya kufungua Mkutano wa Wadau wa Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Patrick Kipangula, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Mbuya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Gerson Msigwa, pamoja na Kamishna na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam. 

Waliosimama nyuma ni viongozi wa Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) akiwemo Muhidin Issa Michuzi (Mdhamini), Mwenyekiti wa TBN Beda Msimbe, Mjumbe Joachim Mushi na Mweka Hazina ambaye pia ni Mtaalamu wa Habari, Cathbert Kajuna.

IMG-20250821-WA0061
Dar es Salaam, Agosti 21, 2025: 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi, ametaja majukumu makuu matano ambayo sekta ya habari nchini inapaswa kuyatekeleza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akisisitiza umuhimu wa taaluma, weledi na maadili katika kuripoti.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Profesa Kabudi alisema vyombo vya habari ni mhimili muhimu katika kukuza demokrasia na kulinda amani wakati wa uchaguzi.

“Vyombo vya habari vinapaswa kuhakikisha wananchi wanajua haki na wajibu wao, kutoa elimu juu ya sera za wagombea, kufuatilia ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, kuhamasisha ushiriki wa makundi maalum kama vijana na wanawake, na kupambana na taarifa potofu badala ya kuzisambaza,” alisema Profesa Kabudi.

IMG-20250821-WA0057
IMG-20250821-WA0059

Aidha, alisisitiza kuwa utekelezaji wa majukumu hayo lazima uongozwe na misingi ya taaluma na maadili ya uandishi wa habari ili kulinda heshima ya tasnia na kuepusha vurugu au uvunjifu wa amani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Wakili Patrick Kipangula, alikumbusha waandishi wa habari kuhakikisha wanakuwa na ithibati kabla ya kufanya kazi za kihabari, hususan katika kuripoti uchaguzi.
IMG-20250821-WA0028
IMG-20250821-WA0031
IMG-20250821-WA0030

“Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari kinasema bayana kuwa mtu yoyote anayetaka kufanya kazi ya uandishi ni lazima awe amepewa ithibati na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari. Hivyo ni kosa la jinai kwa mwandishi wa habari kufanya kazi bila ithibati,” alisema Kipangula.

Aliongeza kuwa uhalali wa waandishi wa habari katika kipindi hiki ni jambo lisiloweza kupuuzia, kwani tasnia hiyo inahusisha majukumu makubwa yanayoathiri utulivu wa taifa.
IMG-20250821-WA0046(1)
Mkutano huo uliwahusisha wadau mbalimbali wa sekta ya habari na utangazaji, ambao walijadili nafasi ya vyombo vya habari katika kulinda maadili ya kitaifa na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

PDPC Yawaasa Mabloga Kulinda Faragha Wakati wa Uchaguzi

Tuesday, August 12, 2025

Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), - Innocent Mungi akitoa mada kuhusu ulinzi wa taarifa binafsi.
Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, akiwasilisha mada katika mafunzo maalumu kuelekea uchaguzi mkuu mahususi kwa bloga yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Agosti 11, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.

DAR ES SALAAM, Agosti 11, 2025 – Waandishi wa habari na mabloga wametakiwa kuelimisha jamii kuhusu sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi, ili kuzuia uvunjifu wa faragha na kuepusha madhara ya kisheria.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Innocent Mungy, wakati wa mafunzo maalum kuelekea Uchaguzi Mkuu, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ombi la Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN).

Mungy alisema mabloga wana nafasi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu sheria hiyo, hasa katika kipindi cha uchaguzi, na kuwaonya kuepuka kuchapisha taarifa binafsi za watu au wagombea.

“Ni kosa kisheria kuingilia mambo binafsi ya watu, na adhabu yake ni kali. Bloga mna wajibu wa kulinda faragha na kuepuka taarifa zinazoweza kuvunja sheria,” alisema Mungy.

Alibainisha kuwa maendeleo ya teknolojia yameongeza fursa na changamoto katika uandishi, hivyo mabloga wanapaswa kutumia majukwaa yao kwa uwajibikaji mkubwa. Pia aliahidi kuchangia mabloga ili waweze kusajili majukwaa yao kama inavyotakiwa kisheria.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Egbert Mkoko, aliwakumbusha washiriki kufuata miongozo rasmi ya uandishi wa habari za uchaguzi, akisisitiza umuhimu wa blogu katika kutoa taarifa sahihi kwa jamii.

Kwa upande wake, Afisa wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Rehema Mpagama, alieleza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuripoti uchaguzi ni wale tu wenye ithibati, kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti wa TBN, Beda Msimbe, aliishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya mafunzo hayo kupitia TCRA, akisema yatasaidia kuongeza weledi na kuimarisha usalama wa taarifa wakati wa uchaguzi.
Mhadhiri katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), Dkt. Darius Mukiza akitoa mada kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Akili Unde (AI)
Afisa wa Kamati ya Bodi ya Ithibati, Rehema Mpagama, akizungumzia Maadili na Sheria kwa Waandishi wa Habari.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Egbert Mkoko, akichangia mada kuhusu Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uandishi wa Habari za Uchaguzi.
Mmilikiwa Blogu ya Michuzi, Issa Michuzi akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Majadiliano yakifanyika.
Wajumbe wa Bodi ya TCRA wakijitambulisha.
Picha ya pamoja.

TCRA Kukutana na Mtandao wa Wanablogu Tanzania Kubainisha Utambulisho wa Wanablogu

Tuesday, August 12, 2025

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kukutana na Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) ili kujadili na kufafanua kwa uwazi nani anastahili kutambulika kama mwanablogu nchini.

Hatua hiyo inafuatia malalamiko ya TBN kwamba wanablogu wa kitaaluma wamekuwa wakichanganywa na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaomiliki akaunti binafsi au za kibiashara, lakini hawana blogu rasmi zenye maudhui ya kitaalamu na muundo maalumu.

Kwa mujibu wa Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, kikao hicho kinatarajiwa kuondoa mkanganyiko uliopo kati ya wanablogu na watengenezaji wa maudhui wengine wa mtandaoni. Amesema maafisa wa TCRA watajadili hoja za TBN, kupitia mfumo wa kisheria uliopo, na kuangalia uwezekano wa marekebisho yatakayozingatia ukuaji wa vyombo vya habari vya mtandaoni nchini.

Mhandisi Kisaka alitoa kauli hiyo wakati wa mafunzo ya wanachama wa TBN kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, yaliyofanyika katika makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam, kutekeleza agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mwenyekiti wa TBN, Beda Msimbe, amesema anaamini kuwa kupitia makubaliano ya pamoja, wanachama wa mtandao huo watapata utambuzi rasmi na nafasi thabiti ya kushiriki katika mijadala ya sera za kidijitali nchini.

Hatua hii inakuja wakati tasnia ya maudhui ya kidijitali ikikua kwa kasi, huku ushawishi wa mitandao ya kijamii, vlogu na tovuti za habari mtandaoni mara nyingi ukifanana, jambo linalofifisha mipaka ya maana halisi ya mwanablogu katika zama hizi za uchumi wa kidijitali.

TCRA yatoa Ratiba ya mafunzo kwa TBN kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sunday, August 10, 2025
WhatsApp%20Image%202025-08-10%20at%2014.04.14

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeandaa mafunzo maalumu kwa Mtandao wa Mabloga  (TBN) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mafunzo haya yatafanyika Jumatatu, Agosti 11, 2025, katika Makao Makuu ya TCRA.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TCRA mafunzo hayo yana lengo la kuwaandaa mabloga na wanahabari kwa ujumla ili waweze kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu. 

Mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalamu kutoka taasisi tofauti. Baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uandishi wa Habari za Uchaguzi, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa za Mwaka 2020, na uhusiano kati ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama.

Mada nyingi zitatoka Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, itakayozungumzia maadili na sheria kwa waandishi wa habari, mada kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na Akili Bandia (AI) kuelekea uchaguzi na mada kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) itakayozungumzia Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuelekea uchaguzi.

Mafunzo haya yana faida kubwa kwa mabloga na jamii kwa ujumla kwani yatawawezesha wanahabari kutoa taarifa sahihi na zenye uwajibikaji, jambo ambalo ni muhimu katika kujenga mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu.

Pia, yanatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na Akili Bandia ili kuepuka taarifa za uongo.

Uchaguzi Mkuu 2025: INEC Yasisitiza Ushirikiano na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni wakiwemo TBN

Tuesday, August 05, 2025

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika leo Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI Mwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele ametoa wito kwa wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuhakikisha taarifa zinazopandishwa katika kurasa zao zinakuwa za kweli na zisizo na chembe ya upotishaji ili kupeuka kuvuruga amani na utulivu wa nchi.

Jaji Mwambegele ametoa wito huo Agosti 3,2025 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi na wazalishaji maudhui mtandaoni kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

"Nawasisitiza na kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kuepuka matumizi mabaya ya akili unde ambayo inatumiwa na baadhi ya watu wenye nia hovu kusambaza habari za upotoshaji hasa kupitia mitandao ya kijamii,"amesema.

Ameongeza kuwa tume hiyo ina matumaini makubwa na vyombo vya habari katika kufanikisha uchaguzi wa mwaka huu kupitia ushiriki wao.

"Imani hii inatokana na ushirikiano wenu mliouonesha tangu awali kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga, mmekuwa wepesi wa kuwasilisha hoja na ushauri pale inapohitajika kila tunapokutana nanyi kwenye vikao,"ameongeza.

Awali akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na ushiriki wa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima amesema Tume inatarajia vyombo vya habari vitatumia kalamu zao na nyenzo walizonanzo kuhubiri amani katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

"Tunawaomba na kuwasihi, kutumia nafasi na fursa mlizonazo kuhakikisha kunakuwepo na taarifa za mara kwa mara za kuelezea kinachoendelea kuhusu uchaguzi, "amesema.

Pia ameongeza kuwa vyombo vya ndivyo vinaweza kuwa sauti ya kwanza ya kuonesha upotoshwaji wa aina yoyote unaofanywa kwa bahati mbaya au makusudi kuhusu Tume na zoezi la uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

"Tume imejiwekea utaratibu wa kuvishirikisha vyombo vya habari katika mchakato mzima wa uendeshaji wa uchaguzi huu ili kuweka uwazi na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu, "ameongeza.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Kailima Ramadhani akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wazalishaji Maudhui Mtandaoni wakiwa katika mkutano wa kitaifa wa Tume Huru wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika Agosti 3, 2025 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
 
Designed By TBN | Developed By Gadiola Emanuel